Uncategorized

MASHINE NYINGINE YA KAZI HII HAPA KUTUA SIMBA

admin April 20, 2020 9:29 pm


IBRAHIM Ame, beki anayekipiga ndani ya Coastal Union naye ameunganishwa kwenye jalada la Bakari Mwamnyeto ambaye inaelezwa anawindwa na Simba.

Ligi ikiwa imesimama kwa sasa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona tayari Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck ameanza kufanya tathimi na kuwataja wachezaji ambao anawakubali ambapo jina la kwanza kutajwa ni la kiungo Lukas Kikoti anayekipiga Namungo huku wengine wakiwa kabatini.

Miongoni mwa nyota ambao wapo kabatini kwenye ripoti inaelezwa kuwa ni pamoja na Ame aliye chini ya nahodha wake Mwamnyeto ambao wamekuwa na muunganiko mzuri ndani ya Coastal Union.

Coastal Union imekubali kuchapwa mabao 19 baada ya kucheza mechi 28 ndani ya Ligi Kuu Bara ikiwa nafasi ya tano na pointi 46.

“Sio Mwamnyeto pekee bali hata yule mwenzake, Ame ni miongoni mwa wanaotazamwa ili kunaswa ndani ya Simba wakati wa usajili ukifika,” ilieleza taarifa hiyo.

Senzo Mazingiza, mtendaji Mkuu wa Simba amesema kuwa kwa sasa sio muda wa kuzungumzia masuala ya usajili wakati ukifika kila kitu kitakuwa wazi.

KIUNGO HUYU ANAYEKIPIGA KENYA AKUBALI KUSAINI YANGA THOMAS PARTEY APIGIWA HESABU KALI NA ARSENAL

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply