Uncategorized

JEMBE ANAAMINI KWAMBA KUTOBOA KWA SAMATTA KUMEFUNGUA NJIA KWA WAZAWA WENGINE KUTAKA KUTOKA NJE

admin April 21, 2020 5:29 pm


KUTOKANA na wachezaji wengi wazawa kupata nafasi ya kucheza nje ya nchi jambo hilo linatoa mwanga kwa wengine kuhitaji kupata nafasi ya kwenda kukipiga pia huko.

Saleh Jembe anasema:”Kidogo wachezaji wa Tanzania, wanaanza kuelewa nini maana ya kucheza nje ya Tanzania, wachezaji wanaanza kupata ari mpya ya kufikiria kucheza nje ya Tanzania.

“Yale mawazo ya kucheza kwenye klabu hizi mbili za Simba na Yanga yanaanza kuyeyuka hili ni jambo zuri na linapaswa liendelee ili kupata wachezaji wengi watakaocheza nje ya nchi.

Jembe amesema kitendo cha baadhi ya wachezaji kufanikiwa kwenda kucheza nje ya Tanzania kwa mafanikio kama Mbwana Ally Samatta, kumewafanya wachezaji wengi wawe na shauku ya kufikiria kutoka nje ya mipaka ya nchi.

CORONA YAMFANYA MORIS KUMKUBUKA KOCHA AZAM COMPLEX SASA MAMBO SAFI, YAINGIA ANGA ZA TP MAZEMBE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply