Uncategorized

GARETH BALE AUKUMBUKA MPIRA

admin April 28, 2020 7:11 am

STAA wa Real Madrid, Gareth Bale amefunguka kuwa anatamani sana kurejea uwanjani, lakini suala la usalama wa afya ni muhimu kwanza.
  Hii ni kutokana na mlipuko wa Virusi vya Corona ambao kwa sasa umeikumba dunia na kusababisha raia kukaa ndani ilikulinda usalama wao.
 Kwa sasa La Liga imesimama kutokana na hali hiyo  toka Machi na bado haijafahamika kuwa itarejea lini rasmi kutokana na  janga hilo.
 “Tumefungiwa ndani huwezi kutoka hata kutembea tu kwa ajili ya mazoezi na hata kufanya mazoezi imekuwa ni ngumu kutokana na hali ya sasa.
“Natamani kuona tunarudi tena uwanjani na sio mimi tu ni wengi wanatamani hivyo, lakini muhimu kuangalia afya zetu kwa sasa sababu Corona ni janga kubwa  nina tumaini kuwa wote tupo vizuri.
“Kitu kigumu kwa sasa unasikia kila mmoja anataka kuona msimu unamalizika, ila ukitafakari kwa umakini unaona kuwa afya za watu ni muhimu kuliko kingine.
“Tumemisi soka kulicheza na hata kuliangalia lakini ndiyo hivyo hakuna kitu kama hicho kwa sasa, ila naamini ipo siku kila kitu kitakuwa sawa,” alisema Bale.
HILI HAPA KOSI MATATA LA WACHEZAJI AMBAO MIKATABA YAO INAMEGUKA MSIMU UKIISHA MANCHESTER UNITED, LIVERPOOL, ARSENAL ZAKUTANA KWA NYOTA HUYU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply