Uncategorized

MCHEKA NA NYAVU MATATA AJIPELEKA YANGA, ATAMBA KUTATUA TATIZO PALE KATI

admin April 29, 2020 10:41 am

DARUES Saliboko, mshambuliaji wa Lipuli amesema kuwa kikosi cha Yanga kinamhitaji mshambuliaji kama yeye ili akatulize eneo la katikati ambalo anaamini huwa linakosa utulivu.


Saliboko anayetupia jezi namba 10 mgongoni amekuwa kwenye ubora wake msimu huu ndani ya Lipuli akiwa ametupia mabao nane ambapo habari zinaeleza kuwa yupo kwenye rada za Yanga.

Akizungumza na Saleh Jembe, Saliboko amesema:”Yanga ni timu kubwa na imara nina amini kinachokosekana pale katikati ni mtu wa kuwatuliza ili wafanye makubwa na iwapo nikaingia pale nitafanya kazi yangu kwa umakini.

“Kingine kinachotakiwa kwa timu kama Yanga ni umakini mkubwa wa wachezaji kwani kila mechi inakuwa na presha kubwa jambo linalowafanya waonekanae kushindwa kufanya kama ilivyokuwa zamani licha ya kuwa ni timu kubwa na yenye nguvu,”.

Yanga ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa imecheza mechi 27 kibindoni ina pointi 51 na imetupia mabao 31 na kinara wao wa utupiaji ni David Molinga mwenye mabao nane.
FEI AWATAKA WATANZANIA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA DUH SASA SIMBA WAMEAMUA KUIPASUA YANGA, KUANZA NA HUYU MTUPIAJI NAMBA MOJA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply