Uncategorized

BOSI HUYU AMESHIKILIA MKATABA WA PACHA HII MATATA NDANI YA YANGA INAYOTUPIWA MACHO NA SIMBA

admin May 1, 2020 7:13 am


IMEEELEZWA kuwa Yanga inasubiri neno kutoka kwa Kocha Mkuu, Luc Eymael ili kumalizana na mastaa walio Kwenye rada zao ambao ni Relliants Lusajo na Lukas Kikoti.

Pacha ya Kikoti na Lusajo imekuwa katika ubora msimu huu 2019/20 ndani ya Ligi Kuu Bara ambapo wamehusika Kwenye mabao 15 kati 34 yaliyofungwa na kosi hilo.

Lusajo ametupia 11 na Kikoti ana mabao manne Kwenye Ligi jambo lililowavutia mabosi wa Yanga na inaelezwa kuwa Simba pia wapo mawindoni kuwawinda nyota hao.

 “Kocha ndiye mwenye maamuzi ambaye anatakiwa kuthibitisha kuwa anahitaji kupata saini zao ama la kisha hesabu za usajili zitaendelea ila sio sasa ni pale muda ukifika,” ilieleza taarifa hiyo.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema:-“Huu sio muda wa usajili mambo bado kabisa hivyo wakati ukifika tutasema nani anaingia na nani anatoka,” .

HAWA HAPA MASTAA 8 WANATAJWA KUWA KWENYE RADA ZA SIMBA. MBELGIJI AANZA NA JINA LAKE SIMBA YAWAOMBA WATANZANIA KUENDELEA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply