Uncategorized

PAMBA SC YAUNGANA NA MBUNGE MABULA KUPAMBANA NA CORONA KWA VITENDO

admin May 1, 2020 1:43 pm

KLABU ya Pamba Sport Club ya Mwanza kwa kushirikiana na Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo la Nyamagana wamekabidhi uongozi wa Soko Kuu Mwanza Mbugani, vifaa  vya kunawia mikono vyenye uwezo wa kubeba lita 800 kudhibiti Virusi vya Corona.

Mwenyekiti wa Pamba Sport Club, Aleem Alibhai amesema klabu hiyo kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana wametoa msaada huo katika Soko Kuu la Mbungani kutokana na ombi maalum la uongozi wa soko hilo ilikuwasaidia wachuuzi, wajasirimali na watumiaji wa soko hilo kuwa na mazingira salama kwa kujikinga na maambukizi ya homa ya Virusi vya Corona.

Naye Mwakilishi wa Mbunge Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula, Bi. Florah Magabe amesema MlMabula anawathamini wananchi wake ambao ni zaidi ya 350,000 na kwa siku ndio wilaya pekee inayohudumia takribani watu 700,000 hadi 1,000,000 kutoka mikoa ya jirani ya kanda ya ziwa pamoja na nchi za maziwa makuu wanaokuja kupata huduma za kijamii Nyamagana.

Mwenyekiti wa Soko Kuu Mwanza, Hamadi Nchora ameshukuru msaada huo na kuomba zaidi taasisi zingine zijitokeze kuwapatia msaada zaidi.

MECHI 100 ZA SALAH ZINA MSOTO WA KUTOSHA BALAA YANGA YAWAOMBA MASHABIKI KUENDELEA KUCHUKUA TAHADHARI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply