Uncategorized

AZAM FC WANATAKA MAJEMBE YA KAZI MATATU

admin May 4, 2020 1:16 pm


ARSTICA Cioaba, Kocha Mkuu wa Azam FC amewaambia mabosi wake kuwa anahitaji kusajili majembe matatu ya kazi kwa ajili ya msimu ujao wa 2020/21.

Miongoni mwa wachezaji ambao walipitishwa na Cioaba ni pamoja na Obrey Chirwa ambaye ameongeza kandarasi ya mwaka mmoja ndani ya mabingwa hao watetezi wa Kombe la Shirikisho.

Ofisa Mtendaji wa Azam FC, Abdulkarim Amin, ‘Popat’ amesema kuwa sababu kubwa ya kuwaongezea mkataba nyota ambao wapo ndani ya Azam FC ni kuendeleza mfumo makini huku hesabu ya kuongeza ikiwa ni kati ya wachezaji watatu.

“Tunahitaji kukifanya kikosi kizidi kuwa bora na chenye mwendo uleule bila kupoteza ile falsafa yake na kwenye upande wa kuongeza wachezaji hatutaongeza wachezaji wengi inaweza kuwa kati ya watatu ila hawatazidi saba.

“Yote ni mapendelezo ya kocha ambaye yeye anajua aina ya wachezaji ambao anawahitaji nasi pia tunawapa nafasi ya kuwa ndani ya kikosi bila hiyana.”

BERNARD MORRISON ATAOA AHADI HII KWA MASHABIKI, AWAOMBA WAENDELEE KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA SIMON MSUVA AMEKUMBUKA KUSHANGILIA BAO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply