Uncategorized

MBRAZILI ANAYETAKA KUCHEZA SIMBA AZIKUMBUKA CHIPSI BONGO

admin May 9, 2020 10:10 am

ANDREY Coutinho, kiungo wa zamani wa Klabu ya Yanga amesema kuwa miongoni mwa vitu anavyovikumbuka kwenye ardhi ya Bongo ni pamoja na chakula alichokuwa akikipata wakati akiwa hapa.

Kiungo huyo amesema kuwa kwa sasa anatamani kurudi Bongo na kucheza ndani ya Simba ama Yanga iwapo watahitaji saini yake.

Coutinho alicheza Yanga msimu wa 2014 aliletwa na Kocha Mkuu wa Yanga wa wakati huo ambaye alikuwa ni raia wa Brazil, Maximo akitokea Klabu ya Taubate SP ya Brazil.

Kiungo huyo amesema:-“Ninakumbuka chakula cha Tanzania kwa namna kilivyokuwa cha kipekee hasa ikiwa ni pamoja na ugali ambao nilikuwa ninaupenda sana licha ya kwamba sikujifunza kupika.

“Pia chips mayai ni aina ya chakula ambacho nilikuwa ninapeda kula kwa kweli nimeikumbuka Tanzania na ninaipenda pia,” amesema.

Kwa sasa kiungo huyo anakipiga ndani ya Klabu ya Ayutthaya United ya nchini Thailand inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.

BANDA AFUNGUKIA ISHU YA LIGI YA AFRIKA KUSINI KUFUTWA KUMBE SANCHO NI BALAA, TIMU KIBAO ZINAMUWINDA IKIWA NI PAMOJA NA MANCHESTER CITY

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply