Uncategorized

MCHEZAJI UTURUKI AMUUA MTOTO, AJIPELEKA POLISI

admin May 14, 2020 1:11 pm

BEKI wa Klabu ya Bursa Yildirim Spor, Cevher Tokts raia wa Uturuki amekiri kumuua mtoto wake kwa kuwa alikuwa hampendi na kujisalimisha polisi.
Tukio hilo, lilitokea Aprili 23, mwaka huu ambapo beki huyo alimpeleka mtoto wake huyo wa miaka mitano hospitali baada ya kuonyesha dalili za Virusi vya Corona.
Lakini baadaye, mchezaji huyo aliwaambia wauguzi kuwa mtoto wake huyo wa kiume alikuwa na tatizo la kushindwa kupumua hivyo alipelekwa Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) na kisha kufariki.
Hata hivyo baada ya siku kadhaa, mchezaji huyo alijipeleka Polisi mwenyewe na kukiri amemua mtoto huyo kwa sababu alikuwa hampendi.
Mchezaji huyo alisema: “Mtoto alikuwa amelala nikachukua mto na kuweka kichwani na kumfumba mdomo kwa dakika 15,” alikiri mwenyewe mbele ya polisi na aliendelea kusema: “Nilikuwa simpendi tangu alipozaliwa na sijui kwa nini na ndiyo maana niliamua kumuua sababu nilikuwa simtaki na sina tatizo lolote la akili.”

Hata hivyo, Polisi wa Uturuki bado wanamshikilia mchezaji huyo na huenda akafungwa maisha.
YANGA YATAJA SABABU YA MABAO 42 YA KAGERE SABABU YA NDOA YA HAJI MANARA KUVUNJIKA YATAJWA, ATAKA KUOA MWINGINE ILA VIGEZO VYAKE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply