Uncategorized

MABEKI HAWA CHIPUKIZI WAPELEKWA DARASANI NA KIRAKA ERASTO NYONI

admin May 15, 2020 4:11 am
ERASTO Nyoni kiraka wa Simba ni miongoni mwa wakongwe ambao muda wote ndani ya uwanja wanafanya vema huku wakiwapeleka darasani mabeki chipukizi wanaokipiga klabu nyingine.

Kennedy Juma ambaye naye anakipiga ndani ya Simba ni miongoni mwa mabeki ambao wanakubali uwezo wa Nyoni.

Dickson Job beki chipukizi anayekipiga ndani ya Klabu ya Mtibwa Sugar amesema kuwa amekuwa akizitazama video za mechi zao dhidi ya Simba huku akijifunza mengi kutoka kwa mkongwe Nyoni.

Bakari Mwamnyeto beki anayekipiga ndani ya Klabu ya Coastal Union naye ni miongoni mwa wanafunzi wa Nyoni ambapo amesema anavutiwa na utendaji wa kazi pamoja na maelekezo yake. “Ni mtu wa kazi ndani ya uwanja hapendi utani hata kidogo muda wote anatoa maelekezo na kufuatilia huku naye akitimiza, pale unapokosea anakuelekeza ili uwe bora, ni darasa tosha kwangu,” amesema Mwamnyeto ambaye alicheza na Nyoni timu ya Taifa ya Tanzania.

ALLY NIYONZIMA AKUBALI KUTUA YANGA NI NDANI YA CHAMPIONI IJUMAA LIPO MTAANI KIPA BIASHARA UNITED AWA BIASHARA KWA MATAJIRI WA BONGO NA KMC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply