Uncategorized

MSHAMBULIAJI WA SIMBA AOMBA NAMBA JUMLA YANGA

admin May 16, 2020 7:58 am

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo ameibuka na kusema anatamani kuona anarejea kuchezea timu kubwa tena nchini ikiwemo Yanga kwani lengo lake ni kutaka kuthibitisha ubora wake.
Mavugo ambaye kwa sasa anakipiga katika Klabu ya Napsa Stars ya Zambia ambapo katika msimu uliopita alifanikiwa kuibuka mfungaji bora, licha ya kucheza Simba kwa msimu miwili lakini hakufanikiwa kuonyesha bora wake kwenye eneo la ufungaji.
Mavugo amesema kuwa kwa upande wake yeye Tanzania ni nyumbani na anatamani kuona akirudi kucheza klabu kubwa ikiwemo Yanga ili kuthibitisha pale ambapo alikosea.

“Suala la kurudi kucheza Tanzania bado lipo kichwani mwangu kwa sababu huko kwangu ni nyumbani, ikitokea nafasi ya kucheza tena kwenye timu kubwa naamini itakuwa ni kitu kikubwa ambacho kila mmoja ataona yupi ni Mavugo.
“Unajua timu kubwa kwa Tanzania zinajulikana kama vile Yanga au Azam nadhani itakuwa sawa kwangu kuweza kuthibitisha kile ambacho kilionekana kuwa kipo tofauti wakati nacheza Simba sasa kama ikitokea ofa nitakubali kuja hata kama ni Yanga,” amesema Mavugo
DILI LA BEKI NKANA KUTUA NDANI YA YANGA LIMEVURUGWA NA MAZAWA HUYU VIDEO: ISHU YA MSHINDI BSS, MADAM RITHA AFUNGUKA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply