Uncategorized

SIMBA YAINGILIA DILI LA MTUPIAJI MGHANA ANAYEWINDWA NA YANGA

admin May 18, 2020 11:28 am


INAELEZWA kuwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wameingia kwenye anga za Yanga kuwania saini ya mshambuliaji Michael Sarpong ambaye hivi karibuni aliachana na klabu ya Rayon Sports ya Rwanda baada ya kuingia kwenye mtafaruku na Rais wa klabu hiyo.

Simba SC wanaripotiwa kuitaka huduma ya Sarpong na sasa wapo katika hatua ya majadiliano na wawikilishi wa mchezaji huyo mwenye miaka 24, ambaye alikuwa mwiba mchungu kwa mabeki wa ligi ya Rwanda tangu alipojiunga na Rayon akitokea Dream FC ya Ghana mwaka 2018.


Vyombo vya habari kutoka Ghana vimeripoti kuwa Simba wameanza hesabu za kuinasa saini ya nyota huyo ambaye aliweka wazi hivi karibuni kuwa Yanga wameanza mpango wa kuisaka saini yake.

Kiwango kikubwa cha Sarpong msimu wa 2018/2019 kiliisaidia Rayon kutwaa ubingwa wa Rwanda Premier League ambapo alifunga magoli 16 na kuibuka mfungaji bora.


 Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liberty Professionals pia alifunga magoli 6 katika kombe la FA msimu huo. Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael inaelezwa kuwa amekubali uwezo wa nyota huyo.

KAGERA SUGAR YAUKUMBUKA MPIRA CHELSEA KUPITISHA PANGA LA KIBABE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply