Uncategorized

YOUNG AHOFIA KUNYOA NYWELE KISA CORONA, AWA NA MUONEKANO WA TOFAUTI

admin May 20, 2020 11:47 am

WINGA wa zamani wa Manchester United, Ashley Young, juzi alionekana akiwa na muonekano wa tofauti baada ya kuacha nywele.
Winga huyo ambaye kwa sasa anaichezea Inter Milan alionekana akiwa tofauti na hali aliyokuwa nayo kwa kipindi kirefu akiwa na Man United kwa kuwa kila mara alionekana akiwa na upara.

Baadhi ya komenti kwenye mitandao ambayo picha hiyo imewekwa zimesema kuwa staa huyo amebaki hivyo kwa kuwa ameshindwa kwenda saluni akiogopa kuambukizwa Virusi vya Corona.
Juzi Inter Milan walianza mazoezi yao na Young alionekana kuwa tofauti na jinsi alivyokuwa awali.
Winga huyo ambaye pia anaweza kucheza beki wa pembeni alijiunga na timu hiyo kwenye usajili wa Januari na ameshaanza kuonyesha kiwango cha hali ya juu.
VIDEO: MOLINGA AFUNGUKA ISHU YAKE YA KUONDOKA YANGA VIDEO:MSHINDI BSS APEWA MILIONI TANO, NYINGINE ZITAKAMILISHWA TARATIBU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply