Uncategorized

LAMPARD ABARIKI KANTE KUJITENGA

admin May 21, 2020 2:17 pm


KOCHA Mkuu wa Chelsea, Frank Lampard amesema kuwa uamuzi wa kiungo wake N’Golo Kante kujitenga na wenzake ni mzuri kwa manufaa yake na afya za wengine pia.

Kante aliripoti mazoezini siku ya Jumanne katika kituo cha Cobham HQ ila alishindwa kurejea siku ya Jumatano kutokana na kutojihisi vizuri.

Kwa sasa timu nyingi zinazoshiriki Ligi Kuu England zimeanza maandalizi ya kufanya mazoezi ya pamoja kwa ajili ya kumalizia mechi zilizobaki baada ya ligi kusimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona .

Habari zinaeleza kuwa sababu kubwa ya Kante kushindwa kuendelea kuripoti mazoezini ni hofu ya kupata maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo bado vinasambaa kwa kasi.

WALE AMBAO WALIKUWA WAMEJISAHAU KUHUSU LIGI MUDA WAO WA KUSHTUKA NI SASA WAJIPANGE MENJA KUNTA AMUONYESHA UDAMBWIUDAMBWI MOLINGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply