Uncategorized

MENJA KUNTA AMUONYESHA UDAMBWIUDAMBWI MOLINGA

admin May 21, 2020 3:17 pm

MWIMBAJI wa muziki wa Singeli nchini Meja Kunta, hivi karibuni alimtoa nishai, straika wa Yanga raia wa DR Congo, David Molinga, kwenye mazoezi yao yaliyofanyika katika Ufukwe wa Escape One jijini Dar es Salaam.
Molinga mwenye mabao nane katika msimamo wa wafungaji wa Ligi Kuu Bara, ameendelea kutoa kauli za kuwaamanisha mashabiki zake wa Yanga kuwa endapo ligi itarejea na kupata nafasi ya kucheza mechi zote, anaweza kumaliza akiwa na zaidi ya mabao 15.
Kwenye mazoezi hayo, Meja Kunta na Molinga walikuwa wakipambana kutokea katika vikosi tofauti hivyo wakajikuta wakipokonyana mpira huku Meja akimpiga Molinga chenga za maudhi na kushangiliwa na baadhi ya mashabiki waliokuwepo ufukweni hapo.
Chenga hiyo ilitoafsiriwa tofauti na baadhi ya wachezaji na mashabiki waliokuwa wakishuhudia mazoezi hayo, na baadhi kuanza kulinganisha ubora wa uchezaji wa Molinga na Meja Kunta, huku wengi wao wakisema msanii huyo akikomaa na soka ana uwezo mkubwa.
LAMPARD ABARIKI KANTE KUJITENGA MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply