Uncategorized

YANGA MGUU SAWA KUELEKEA LIGI KUU BARA

admin May 26, 2020 3:47 pm

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa mastaa wote wa timu hiyo waliopo Tanzania wataingia kambini mapema kabla ya kuanza mazoezi ya pamoja kuanza kuelekea kwenye mechi za Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza kutimua vmbi Juni Mosi.

Ligi Kuu Bara ilisimamishwa Machi 17 kutokana na janga la Viriusi vya Corona ambavyo vinaitikisa dunia na inatarajiwa kurejea hivi karibuni baada ya Serikali kusema kuwa hali ya maambukizi imeanza kupungua.

Akizungumza na Seleh Jembe, Ofisa Uhamasishaji na Msemaji wa Klabu ya Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa wana imani wachezaji wote wataingia kambini kwa wakati.

“Wachezaji wengi wote wapo nchini isipokuwa mmoja tu Farouk Shkalo yeye yupo Kenya utaratibu unafanyika ili aweze kurejea.

“Kwa upande wa benchi la ufundi ni mpaka pale mambo yatakapokuwa shwari kwani huko kwao mipaka bado haijafunguliwa itakapofunguliwa tu watarejea kuungana na timu,” amesema.

Leo mastaa wa klabu hiyo baadhi wameanza kuripoti ambapo wanatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya.

SAFARI YA MABADILIKO YANGA YAPAMBA MOTO LIPULI FC YAPIGIA HESABU 10 BORA NDANI YA LIGI KUU BARA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply