Enock Morrison Yanga Simba
Habari za michezo

Enock Morrison Afichua Ukweli Mzito Kuhusu Yanga na Simba

Vardo November 14, 2026 7:31 pm

Kiungo mshambuliaji matata wa Al-Merrikh SC ya Sudan, Mghana Enock Morrison, ameweka wazi kuwa bado ana ndoto za kuja kuchezea klabu kubwa za Tanzania, Yanga SC au Simba SC, licha ya dili lake la kujiunga na wekundu wa Msimbazi kuota mbawa msimu uliopita.

Katika mahojiano maalum akiwa nchini Sudan, Morrison alithibitisha kuwa mbali na Singida Black Stars kuonyesha nia ya dhati ya kumuhitaji, Simba SC ilikuwa hatua za mwisho kumsajili baada ya mkataba wake na Gor Mahia ya Kenya kumeguka mwishoni mwa msimu wa 2025-2026, kabla ya mazungumzo kukwama kwenye baadhi ya vipengele vya mkataba.

“Yanga na Simba ni timu kubwa na zenye ushindani mkubwa sana ukanda wa Afrika Mashariki na hata barani Afrika kwa ujumla. Kila mchezaji mkubwa anatamani kucheza hapa, na bado nina malengo hayo ya kucheza Tanzania siku moja,” alisema nyota huyo.

Rekodi na Uwezo Wake Uwanjani

Nyota huyo aliyezaliwa Januari 18, 2000, ana uwezo mkubwa wa kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji wa kati pamoja na kutokea pembeni. Amepitia vilabu mbalimbali vikubwa vikiwemo King Faisal FC na Asante Kotoko za nchini kwao Ghana.

Morrison anaingia kwenye kumbukumbu kama mchezaji wa kigeni aliyetwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Kenya (MVP) baada ya miaka 14, akimfuata Mganda Dan Sserunkuma aliyeweka rekodi hiyo mwaka 2012. Nyota huyo aliongoza Gor Mahia kubeba ubingwa wao wa 22, akihusika kwenye mabao saba (kufunga 3 na kutoa pasi 4 za mabao) katika mechi 31 alizocheza msimu wa 2025-2026.

Geita Gold Yafungua Milango kwa Nyota wa Zamani wa Simba, Ladack Chasambi!