Uncategorized

WACHHEZAJI SIMBA WATIA TIMU MO ARENA KWA AJILI YA MAZOEZI

admin May 27, 2020 1:47 pm


KIKOSI cha Simba leo kimetia timu katika uwanja wa Mo Arena kuanza kufanya mazoezi kwa ajili kuanza maandalizi kuelekea kwenye mechi za Ligi Kuu Bara.

Wachezaji wa Simba wameripoti leo kambini na kufanyiwa vipimo vya afya pamoja na maelekezo mengine kuhusu kujilinda na Virusi vya Corona.

Leo inakuwa ni mara ya kwanza kwa wachezaji wa Simba kufanya mazoezi kwa pamoja baada ya masuala ya michezo kusimamishwa Machi 17 na Serikali kutokana na janga la Virusi vya Corona.



Baadhi ya nyota ambao wamewasili ni pamoja na Pascal Wawa, Jonas Mkude, Meddie Kagere, Gadiel Michael, Shomari Kapombe, Aish Manula na Tairone Santos.

Serikali imeruhusu masuala ya michezo kuanza Juni Mosi.

POLISI TANZANIA YAANZA MAZOEZI RASMI AZAM FC WAPO TAYARI KWA AJILI YA LIGI, WAENDELEA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply