Uncategorized

AZAM FC WAPO TAYARI KWA AJILI YA LIGI, WAENDELEA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA

admin May 27, 2020 2:47 pm


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya kuendelea na msimu wa Ligi Kuu Bara.


Serikali ilisimamisha masuala ya michezo Machi 17 kuzuia mijumuiko isiyo ya lazima kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona tayari imeruhusu masuala ya michezo kuendelea ifikapo Juni Mosi.


Ofisa Habari wa Azam FC, Zaka Zakazi amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya kuona ligi ikirejea na maandalizi yanatarajia kuanza hivi karibuni huku wakiendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

Azam FC imeweka mtambo maalumu wa kujitakasa kwa wachezaji, wale watakaotembelea uwanja huo pamoja na wafanyakazi wa hapo ili kuendelea kulinda afya ambayo ni utajiri namba moja.

Leo wameanza mazoezi rasmi kwa ajili ya kujiaandaa na mechi zao zilizobaki ndani ya ligi.

WACHHEZAJI SIMBA WATIA TIMU MO ARENA KWA AJILI YA MAZOEZI KAZI TAYARI IMEANZA YANGA, SIMBA NAKO KUMENOGA, KESHO NDANI YA SPOTIXTRA ALHAMISI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply