Michezo

ARNE SLOT AINGIA RADA ZA AC MILAN

Vardo May 31, 2026 3:46 pm

LONDON ENGLAND: Kocha Arne Slot ameibuka kama mmoja wa wagombea wanaotajwa kuchukua nafasi ya kuinoa AC Milan baada ya kuondoka katika klabu ya Liverpool.

Klabu hiyo ya Italia inatafuta kocha mpya baada ya kumfuta kazi Massimiliano Allegri, ambaye anatarajiwa kujiunga na Napoli.

Milan tayari imefanya mazungumzo na Andoni Iraola, ambaye anatajwa kuwa ndiye anayetarajiwa kuchukua nafasi ya Slot Liverpool. Hata hivyo, Iraola amekuwa akisubiri kuwasiliana na mkurugenzi wa michezo wa Liverpool, Richard Hughes.

Klabu hiyo ya Italia pia imepanga kukutana na Oliver Glasner mapema wiki hii huku ikiendelea na mchakato wa kutafuta kocha mpya.

Glasner anatarajiwa kuondoka katika Crystal Palace kama kocha huru baada ya kuiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa UEFA Europa Conference League kwa kuifunga Rayo Vallecano kwenye fainali.

Crystal Palace pia ilikuwa imempa ofa Iraola na ilikuwa ikisubiri majibu yake mwishoni mwa wiki kabla ya taarifa za kuondoka kwa Slot kutoka Liverpool kujulikana Jumamosi asubuhi.

Inaelezwa kuwa AC Milan haihitaji ruhusa kutoka Liverpool ili kufanya mazungumzo na Slot, kwa kuwa masharti ya kuondoka kwake yanamruhusu kuzungumza na klabu yoyote. Hata hivyo, swali kubwa ni kama kocha huyo raia wa Uholanzi yuko tayari kurejea kazini mara moja au atahitaji muda wa kupumzika kwanza.

Mbali na Allegri, Milan pia imefanya mabadiliko makubwa katika uongozi wake baada ya kushindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Klabu hiyo iliwafukuza mkurugenzi wa michezo Igli Tare, mtendaji mkuu Giorgio Furlani na mkurugenzi wa ufundi Geoffrey Moncada siku moja baada ya kukosa tiketi ya Ligi ya Mabingwa.

Kwa sasa, mkurugenzi wa zamani wa michezo wa Tottenham Hotspur na Barcelona, Ramon Planes, ndiye anayeonekana kuwa mgombea mkuu wa kuwa mkurugenzi mpya wa michezo wa AC Milan.

SIMBA WAAHIDI MAJINA MAZITO, STRAIKA MPYA KUONGEZA NGUVU MEXICO KUJARIBU SIRAHA ZAKE DHIDI YA AUSTARIA