Uncategorized

AMEBAKI SHIKALO TU KUREJEA YANGA KWA SASA

admin May 28, 2020 3:47 pm


WACHEZAJI wote wa Klabu ya Yanga tayari wameripoti kambini na kuanza kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mechi zilizobaki za Ligi Kuu Bara.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa ni mchezaji mmoja tu ambaye hayupo kambini kwa sasa kutokana na kukwama nchini Kenya ambapo mipaka imefungwa.

“Wachezaji wote wameripoti kambini isipokuwa Shikalo yeye yupo Kenya, imekuwa ngumu kuripoti kwa sasa kutokana na mipaka ya huko kufungwa kutokana na tahadhari dhidi ya ya Virusi vya Corona ila mambo yakiwa sawa atarudi muda wowote kuanzia sasa,” amesema. 

Machi 17 masuala ya michezo yalismamishwa na Serikali kutokana na kusambaa kwa kasi kwa Virusi vya Corona jambo lililopeleka wachezaji kupata mapumziko ya lazima.

SABABU YA MEDDIE KAGERE KUWEKWA KWENYE RADA ZA TIMU YA HISPANIA HII HAPA KAHATA MAMBO BADO NCHINI KENYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply