Uncategorized

ICARD KUBAKI NDANI YA PSG

admin May 30, 2020 6:47 am

MSHAMBULIAJI wa Inter Milan, Mauro Icard anayekipiga kwa mkopo ndani ya Paris Saint-Germain (PSG) inaelezwa kuwa anataka kubaki jumla ndani ya timu hiyo.

Raia huyo wa Argentina, alijiunga na mabingwa wa Ligue 1 mwanzoni mwa msimu wa 2019-20 akitokea Inter Milan amecheza jumla mechi 31 na kutupia mabao 20.

Bosi wa PSG Thomas Tuchel, inaelezwa kuwa ameanza mpango wa kufanya naye mazungumzo ili abaki ndani ya kikosi hicho.

Mshambuliaji huyo amekuwa ni mbadala wa Edinson Cavan wakati alipokuwa na majeraha kabla ya masuala ya michezo kusimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona.


Amekuwa na muunganiko mzuri ndani ya kikosi wakiunga utatu wao dhidi ya Kylian Mbappe na Neymar ambao wote ni washambuliaji.

YANGA,KOTEI MAMBO SAFI,NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI SVEN: TARATIBU WACHEZAJI WATAREJEA KWENYE UBORA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply