Uncategorized

SIMBA:MECHI YETU DHIDI YA AZAM FC NI YA KISASI

admin May 30, 2020 5:47 am


UONGOZI wa Simba umesema kuwa mechi yao ya Kombe la Shrikisho hatua ya robo fainali dhidi ya Azam FC itakuwa ni ngumu na ya kisasi.

Jana, ratiba ya hatua ya robo fainali ilipangwa ambapo Simba itakutana na Azam FC ambao ni mabingwa watetezi wa kombe hilo walilolitwaa kwa kuitwanga Lipuli FC bao 1-0.

Sven Vandernbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anaamini utakuwa mchezo mgumu kutokana na Azam FC kuwa ni mabingwa watetezi na waliwafunga walipokutana kwenye mechi ya ligi.

“Utakuwa ni mchezo mgumu ukizingatia kwamba Azam FC tuliwafunga kwenye mechi yetu tulipokutana hivyo watajipanga kulipa kisasi.

“Tunajiandaa vizuri ili kuona namna gani tutapata matokeo kwani kila mechi kwetu tunachotazama ni matokeo,” amesema.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Juni 27 Uwanja wa Taifa, mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi kati ya Yanga ama Kagera Sugar.

CHEKI MOTO WA KIKOSI BORA CHA MSIMU WA 2019/20 YANGA,KOTEI MAMBO SAFI,NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply