Uncategorized

MAJEMBE MANNE YA KAZI YANGA FRESH, MUDA WOWOTE KUTUA BONGO

admin June 4, 2020 6:47 am


MAJEMBE manne ya kazi yameruhusiwa kutua Yanga kukipiga msimu ujao iwapo mambo yatakwenda sawa.

Majembe hayo yanakipiga ndani ya Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda ambao ni Michael Sarpong, Ally Niyonzima, Jules Ulimwengu na Fabrice Mugheni.

Nyota hao kwa sasa wanaweza kutua Bongo kwa kuwa Shirikisho la Soka Rwanda,(Ferwafa) limemaliza msimu mazima kwa kuipa ubingwa APR na kuwafanya wachezaji wanaomaliza mikataba kuwa huru kusepa.

Habari zinaeleza kuwa muda wowote wanaweza kuja kuongea na Yanga ila kitakachowachelewesha ni suala la mipaka ambayo bado imepigwa pini kutokana na kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.


 “Wanaweza kuja wakati wowote kwa kuwa Ligi Kuu ya Rwanda imefutwa, kitkachowazuia kuja mapema ni mipaka kufungwa ila mambo yakiwa sawa watakuja,” ilieleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi na Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said amesema kuwa iwapo wanahitaji kumpata mchezaji hawawezi kushindwa.

AZAM FC YAIVIMBIA SIMBA KIMTINDO MKULIMA WA MPUNGA ATOA AHADI KUBWA NDANI YA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply