Uncategorized

NDANDA KESHO KUTESTI MITAMBO NA NAMUNGO

admin June 5, 2020 10:47 am


KOCHA wa timu ya Ndanda FC, Meja mstaafu Abdul Mingange amesema kuwa kikosi chake kimeanza mazoezi vizuri jambo ambalo anaamini kwamba kitafanya vizuri kwenye mechi zake za ushindani.

Kesho, Ndanda FC itamenyana na Namungo FC kwenye mchezo wa kirafiki utakaopigwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona huku kiingilio ikiwa ni buku mbili.

“Tupo sawa na tumejipanga kuona kwamba kikosi kinafanya vema kutokana na ugumu uliopo kwenye ushindani wa Ligi Kuu Bara.

“Kila mchezaji ana kazi kubwa ya kufanya kwenye ligi na ushindani ambao upo nina amini kwamba tutakuwa vizuri kwani kwenye mazoezi kuna jambo ambalo nimeliona hivyo tukicheza mchezo wa kirafiki tutazidi kuwa imara,” amesema.

MTIBWA SUGAR: TUPO TAYARI KUREJEA KWENYE USHINDANI SVEN: WACHEZAJI WAPO VIZURI, BADO TUNAENDELEA KUWAREJESHA KWENYE UBORA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply