Uncategorized

NDANDA FC INAHITAJI MILIONI 48 IBAKI NDANI YA LIGI

admin June 6, 2020 9:47 am


KLABU ya Ndanda FC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Meja mstaafu Abdul Mingange inahitaji kiasi cha shilingi milioni 48 kutoka kwa wadau ili kiweze kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara msimu ujao.


Mkuu wa Mkoa wa Mtwara abaye ni mlezi wa Ndanda FC, Gelasius Biakanwa amesema kuwa wanahitaji fedha hizo kutoka kwa wadau ili wazitumie kwenye gharama za timu.

“Pesa ninayohitaji haipungui shilingi milioni 48, ninaomba wadau wa michezo waanze kuchangia fedha hizo ambapo ni kwa ajili ya ajili ya posho za wachezaji pamoja na safari.

“Lengo ni kuona timu inabaki ndani ya ligi kwani haiwezi kubaki iwapo hakutakuwa na fedha, kwa wadau ambao wameanza kuchangia ninawashukuru,” amesema.

Ndanda FC ipo nafasi ya 16 ikiwa na pointi 31 baada ya kucheza mechi 29.

SABABU YA AZAM FC KUCHEZA TRANSIT CAMP YAFAFANULIWA KITAALAMU NA CIOABA YANGA WAINYOOSHA MABAO 2-0 DAR CITY

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply