Uncategorized

FA KUFUNGUA DIRISHA LA USAJILI AGOSTI

admin June 9, 2020 6:47 am


CHAMA cha Soka England (FA) kipo kwenye mchakato wa kufungua dirisha la usajili itakapofika Agosti mpaka kufika tamati Oktoba.

Mpango mkubwa wa kufungua dirisha la usajili ambao ulikuwepo tangu awali ilikuwa ni kuufungua Juni 8 ila ililishindikana kutokana na janga la Virusi vya Corona kutibua mambo.

Msimu 2019-20 ambao ulisimamishwa tangu Machi 13 unatarajiwa kuendelea Juni 17 jambo linalofanya klabu nyingi kushindwa kuanza kufanya usajili kwa kuwa bado kuna mechi zimebaki mkononi mwao.

Shirikisho la Soka duniani (FIFA) lipo kwenye mpango wa kuandaa utaratibu ambao utatumika pindi dirisha la usajili litakapofunguliwa.

Miongoni mwa wachezaji ambao wanatajwa kuwa kwenye hesabu za kusepa ndani ya timu zao ni pamoja na Raheem Sterling anayekipiga Manchester City, Pierre Aubameyang mshambuliaji wa Arsenal.

KANTE NA JORGINHO WAPO KWENYE MPANGO WA KUUZWA BREAKING: SIMBA YATOA TAMKO KUHUSU WACHEZAJI WAKE KUSEPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply