Uncategorized

MIRAJI AINGIA KATIKA REKODI

admin June 15, 2020 5:47 am

 MIRAJ Athumani, ameingia kwenye rekodi kuwa mchezaji wa kwanza wa Simba kufanyiwa mabadiliko ya nne kwa mara ya kwanza katika Klabu ya Simba.

Kabla ya mabadiliko kwa mujibu wa sheria za Fifa ni awali ilikuwa ni matatu lakini baada ya ugonjwa wa Corona, Fifa imeruhusu kwa dharura mabadiliko matano.


 Katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting jana, Juni 14 Uwanja wa Taifa, Simba ilifanya mabadiliko manne, Miraji maarufu kama Sheva akaingia kuchukua nafasi ya Miquissone raia wa Msumbiji.

Mpaka dakika 90 zinakamilika mchezo ulikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1. Lile la Simba lilifungwa na Shiza Kichuya na kwa Ruvu Shooting lilifungwa na Fully Maganga.

MNYARWANDA ANAYETAJWA KUWINDWA NA YANGA AWAAGA MASHABIKI RASMI BERNARD MORRISON AKIRI ALIPOKEA FEDHA KUTOKA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply