Uncategorized

ISHU YA OKWI KUREJEA SIMBA IMEIVA

admin June 30, 2020 9:47 pm


NYOTA wa zamani wa Klabu ya Simba, Emanuel Okwi inaelezwa kuwa yupo njiani kurejea ndani ya Klabu ya Simba ambayo aliitumikia msimu wa 2018/19 wakati wakitwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo.

Okwi amekuwa na mahusiano mazuri na Kagere ndani ya Simba pamoja na wachezaji wengine ikiwa ni pamoja na Clatous Chama ambaye ni kiungo kipenzi cha mashabiki wa Simba.

Habari kutoka ndani zinaeleza kuwa tayari mchezaji huyo amekubali kurejea ndani ya Simba ili kuendelea kufanya kazi aliyoimaliza msimu wa 2018/19 wakati alipoibukia nchini Misri.

Raia huyo wa Uganda ambaye anavaa jezi namba 7 hata kwenye timu ya Taifa ya Uganda mgongoni kwa sasa anaitumikia Klabu ya Al Ittihad ya Misri.

“Yupo njiani kurejea ndani ya Simba na kila kitu kipo sawa ni suala la kusubiri tu mambo yakamilike ili atue tena Simba,” ilieleza taarifa hiyo.

Hivi karibuni Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa alisema kuwa mpango wa kusajili unategemea ripoti ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck.

TIMU YA ALLIANCE GIRL’S YAPATA AJALI BERNARD MORRISON NI PASUA KICHWA NDANI YA YANGA, ATIMKA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply