Uncategorized

MABINGWA WA LIGI KUU BARA WATAJA WANAOSTAHILI KUSHUKURIWA KWA TAJI LAO LA 21, WAKABIDHIWA KOMBE LINDI

admin July 8, 2020 3:47 pm


UONGOZI wa Simba umesema kuwa shukran kubwa za kutwaa ubingwa wanazirejesha kwa Mungu pamoja na mashabiki wa Klabu hiyo kwa kuipa sapoti mwanzo mwisho.

Leo Simba imekamilisha safari ya kukabidhiwa ubingwa wao Kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Majliwa.

Mchezo huo umekamilika kwa sare ya bila kufungana na kuwafanya Simba wasepe na pointi mbili nyanda za juu Kusini baada ya mchezo wa kwanza kulazimisha sare ya bila kufungana na Ndanda FC, Uwanja wa Nangwanda Sijaona. 

Ofisa Habari wa Simba,  Haji Manara amesema kuwa anaamini ni mpango wa Mungu kutwaa ubingwa pamoja na sapoti kubwa ya mashabiki.

“Wamekuwa nasi bega kwa bega mashabiki kwenye kazi kubwa ambayo wachezaji walikuwa wakifanya kwa namna yoyote ile wanahitaji pongezi na wanastahili  haya tunayoyapata kwa sasa,” amesema. 

Huu ni ubingwa wa 21 kwa Simba inayonolewa na Sven Vandenbroeck,  na Kocha Msaidizi Seleman Matola.

VPL: KAGERA SUGAR 0-0 YANGA KESHO NDANI YA GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply