Uncategorized

HUU NDIO MKWANJA WATAKAOVUNA SIMBA NA YANGA KESHO IKIWA WATASHINDA

admin July 11, 2020 2:47 pm


 KUELEKEA dabi ya Jumapili, itakayopigwa Uwanja wa Taifa, kati ya Simba na Yanga mabosi wa Simba wameweka ahadi  ya Sh Mil 400 kwa wachezaji wake huku Yanga wakiweka mezani sh Mil 200.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka gazeti la Championi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba, Mohammed Dewji pamoja na viongozi wake wameweka ahadi ya Sh Mil 400 kwa wachezaji wake kama watafanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya Yanga.

Hivyo katika mgawo huo kila mchezaji atayecheza ataondoka na sh Mil 20,watakaotokea benchi sh Mil 10 watakaokaa benchi bila kucheza sh Mil 7,huku wale ambao hawatacheza wataambulia sh Mil 5.

Kwa upande wa Yanga kampuni ya GSM wameweka ahadi kama ile ya kwanza ya Sh Mil 200 huku kukiwa na nyongeza ya ahadi kama watafanikiwa kuifunga Simba.

Hivyo kama Yanga watafanikiwa kuibuka na ushindi katika mechi hiyo kila mchezaji atayeanza atafanikiwa kuvuna Sh Mil 10,wachezaji wa akiba watapata Sh Mil 5 na wale watakaokaa jukwaani watapata Sh Mil 2.

MTUPIAJI NAMBA MOJA KWA WAZAWA AFUNGUKA ISHU YAKE NA KOCHA MKUU PAMOJA NA WACHEZAJI NAMUNGO FC YATINGA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO, YAMSUBIRI MSHINDI WA MCHEZO WA SIMBA NA YANGA KESHO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply