Uncategorized

KOCHA YANGA AMBAKISHA KIKOSINI MTUPIAJI NAMBA MOJA, DAVID MOLINGA

admin July 19, 2020 9:47 pm


MWINYI Zahera, kocha wa zamani wa Yanga amesema kuwa anatamani kuona  David Molinga akiendelea kubaki kuichezea Yanga msimu ujao kwa kuwa ni mchezaji mzuri ambaye kiwango chake kinafanana na Meddie Kagere na John Bocco wa Simba.

Molinga ni kinara wa mabao katika kikosi cha Yanga baada ya kufunga mabao 10 huku Kagere akiongoza kwa kufumania nyavu kwa kuwa na mabao 22 hadi sasa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Zahera alifunguka kuwa, Molinga ni miongoni mwa wachezaji wenye kiwango cha juu ndani ya Yanga ambaye anahitaji kupewa nafasi ili aweze kufumania nyavu kwa kuwa kiwango chake kinafanana na Kagere na Bocco.

“Watu wengi walisema Molinga hafai, huyu ni mchezaji mzuri anaweza kuisaidia Yanga, kocha anatakiwa amuelewe Molinga ni mchezaji wa aina gani, anacheza vipi, ufungaji wake hautofautiani na Kagere na Bocco.

“Nilisema atafunga mabao mengi akipewa nafasi atafanya vizuri zaidi, takwimu ya mchezaji ndiyo inayoonyesha kama ni mchezaji mzuri ama mbaya.
“Anatakiwa amjue ni mchezaji wa aina gani afanyishwe mazoezi ya kufika ndani ya boksi ili aweze kufunga mabao mengi, alikuwa anawekwa benchi hapati nafasi ya kucheza ndiyo maana alishindwa kuonyesha kiwango chake hapo nyuma,” alisema Zahera.
KUMEKUCHA YANGA, MAJEMBE HAYA MANNE YA KAZI KUSEPA MAZIMA SIMBA YATOA TAMKO KUHUSU HATMA YA LUIS NDANI YA KIKOSI HICHO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply