Uncategorized

NDEMLA AIMALIZA ALLIANCE KWA KUKAMILISHA 5G TAIFA

admin July 19, 2020 4:47 pm


SAID Ndemla, kiungo wa Simba leo amefunga bao lake la kwanza ndani ya msimu wa 2019/20 akimalizia pasi ya kiungo mwenzake Hassan Dilunga na kuonyesha lile tabasamu lake la siku zote.

Simba leo, Julai 19 imeshinda mabao 5-1 mbele ya Alliance FC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Mtupiaji namba moja wa Simba na ligi, Meddie Kagere alianza kufunga dakika ya 24 kwa penalti lilisawazishwa na Martin Kigi wa Alliance dakika ya 38.

Bao hilo lilidumu kwa muda wa dakika sita, dakika ya 44 Kagere alitupia bao la pili na kumfanya afikishe jumla ya mabao 22 kwa sasa.

Nyota wa mchezo wa leo Luis Miqussone alifunga dakika 63,  Deo Kanda dakika ya 66 na msumari wa Ndemla kiungo wa Simba ukimaliza hesabu dakika ya 87.

Ushindi huo unaifanya Simba izidi kujikita kileleni ikiwa na pointi 84 kibindoni huku Alliance ikiwa nafasi ya 17 na pointi zake 41 zote zimecheza jumla ya mechi 36.


BOXER APEWA SOMO NA NAHODHA WA YANGA LIPULI YAGAWANA POINTI MOJAMOJA NA AZAM FC SAMORA,IRINGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply