Uncategorized

YANGA WATAJA SABABU YA KUZITAKA POINTI TATU ZA MTIBWA SUGAR LEO

admin July 21, 2020 9:47 pm
UONGOZI wa Klabu ya Yanga umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa leo, Julai 22 dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. 

Yanga imeshatia timu Morogoro na jana ilifanya mazoezi kwa ajili ya mchezo ambao ni muhimu kwao kwa kuwa wanahitaji pointi tatu kama ilivyo kwa Mtibwa Sugar.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kikubwa ambacho wanakihitaji ni kumaliza nafasi ya pili ili kuongeza heshima. 

“Tunawaheshimu wapinzani wetu Mtibwa Sugar na tunatambua kwamba wanapambana kubaki ndani ya Ligi kutokana na kutokuwa na mwenendo mzuri kwa sasa.

“Tunahitaji pointi tatu kuongeza nafasi ya kubaki hapa tulipo hivyo mashabiki wajitokeze kutupa sapoti Kwenye mchezo wetu mgumu,” amesema. 

Yanga ipo nafasi ya pili na ina pointi 68 huku Mtibwa Sugar ikiwa nafasi ya 14 na pointi 41 haina uhakika wa kubaki ndani ya Ligi ikiwa itapoteza mchezo wake mbele ya Yanga.

KAZI IMEANZA SIMBA, NYOTA SABA KUSEPA KIKOSINI MSIMU UJAO HAPA NDIPO AMBAPO GARI LA AZAM FC LITAPAKI KUSEPA NA WACHEZAJI HAWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply