Uncategorized

MKALI WA KUMWAGA MAJI NDANI YA AZAM FC KUIKOSA MBEYA CITY LEO

admin July 23, 2020 12:47 pm


NICHOLAS Wadada, beki wa Azam FC, leo ataukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex dhidi ya Mbeya City, majira ya saa 1:00 jioni.

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati amesema kuwa nyota huyo raia wa Uganda anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi cha leo.

“Wadada hatakuwa sehemu ya kikosi cha leo kwa kuwa ana kadi tatu za njano hivyo atatumikia adhabu yake hiyo lakini hakuna kitakachoharibika.

“Kuna wachezaji wengi na wazuri ambao wana uwezo wa kufanya kazi kama yeye ndio maana halisi ya timu, tunahitaji ushindi ili kufufua matumaini ya kumaliza Ligi Kuu Bara nafasi ya tatu,” amesema.

Wadada ametoa jumla ya pasi saba za mabao huku yeye akipachika bao moja ndani ya Azam FC iliyo nafasi ya tatu na pointi 66.

Azam FC Inapambania nafasi ya pili na Yanga ambayo ina pointi 69 kibindoni kwa sasa baada ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar jana, Julai 22, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

KIKOSI CHA SIMBA LEO DHIDI YA COASTAL UNION KILICHO NYUMA YA UWEZO WA KIPA NAMBA TATU WA YANGA HIKI HAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply