Uncategorized

BARNES AINGIA ANGA ZA LIVERPOOL

admin July 26, 2020 10:47 am


HARVEY Barnes, kiungo wa Leicester City ripoti zinaeleza kuwa yupo kwenye rada za mabingwa wa Ligi Kuu England, Liverpool.

Kocha Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp inatajwa kuwa kinachomvutia kwa nyota huyo mwenye miaka 22 ni spidi ndani ya uwanja pamoja na nguvu.

Licha ya mabosi wa Leicester City ambao wanatumia Uwanja wa King Power kudaiwa kuweka ugumu kwa ajili ya nyota huyo Liverpool imejipanga kuongeza ushawishi ili kupata saini yake.

Mpango mkubwa wa Klopp ni kuimarisha kikosi chake huku akilenga kumuandaa Barnes kuwa mbadala wa Sadio Mane ambaye inaelezwa kuwa Real Madrid wanaiwinda saini yake.

Miongoni mwa majina ambayo yameishtua Leicester City ni pamoja la nyota huyo kutajwa kuwa kwenye rada za Liverpool.

HUKO ENGLAND NAKO VITA YA KUSHUKA DARAJA NI MBICHI, ASTON VILLA KAZI IPO MWAKALEBELA: MKAPA ALIKUWA MTU WA MICHEZO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply