Uncategorized

MOHAMED SALAH YEYE ANA BALAA KWA MISHUTI

admin July 26, 2020 6:47 am


 Mohamed Salah mshambuliaji wa Liverpool kwa msimu wa 2019/20 amekuwa ni mzuri kwenye kupiga mashuti kuelekea lango la wapinzani kwa kuwa kazi yake ni kutafuta lango lilipo.

Amepiga jumla ya mashuti 129 akiwa ni kinara kwa wachezaji wanaoshiriki Ligi Kuu England ambayo inafika tamati leo Julai 26 na inatarajiwa kuanza Septemba 12 kwa msimu wa 2020/21.

 Raia huyo wa Misri kibindoni amefunga jumla ya mabao 19 na timu yake tayari imeshatwaa ubingwa wa Premier ikiwa chini ya Jurgen Klopp.

Leo Liverpool inamaliza kazi mbele ya Newcastel itakuwa ugenini kusaka pointi tatu na ikifanikiwa kushinda itafikisha jumla ya pointi 99 kwa kuwa sasa kibindoni ina pointi 96.

AZAM FC WANA JAMBO LAO KWENYE USAJILI MSIMU UJAO KIUNGO WA YANGA KUIBUKIA AZAM FC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply