Uncategorized

SIMBA YAJIFUA LEO SUMBAWANGA KUELEKEA MCHEZO WA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO

admin July 31, 2020 6:47 pm

KIKOSI cha Simba leo kimefanya mazoezi kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa Shule ya  St. Maurus ikiwa ni maandalizi ya kuelekea mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Namungo FC. 

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Agosti 2, Uwanja wa Nelson Mandela unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili.

Simba ipo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck na Namungo FC ipo chini ya Kocha Mkuu Hitimana Thiery.

Sven amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na anaamini mchezo utakuwa mgumu licha ya wengi kuipa nafasi timu yake kushinda.

Thiery amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo licha ya wachezaji wake wengi kusumbuliwa na typhoid na Malaria.

Namungo ina tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho kwa kuwa Simba inaiwakilisha nchi Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutwaa taji la Ligi Kuu Bara.

NIYONZIMA ALIYEKUWA ANAWINDWA NA YANGA ANUKIA AZAM FC YANGA WAMEAMUA SASA, WAMALIZANA NA MASHINE YA KAZI YA AS VITA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply