Uncategorized

RUVU YAPIGA PANGA WATANO

admin August 5, 2020 3:47 pm

Benchi la ufundi la timu ya Ruvu Shooting Star,  limeacha wachezaji *watano* ambao walikuwemo katika kikosi cha timu hiyo msimu wa 2019/20.

Aidha benchi hilo la ufundi linaloongizwa na kocha *Salum Mayanga* limeshauri, pamoja na wachezaji waliokuwepo ambao mikataba yao haijamalizika na wale waliomaliza mikataba yao, ambao wako katika mazungumzo ya mwisho ya
kukamilisha usajili wao, wasajiliwe *wachezaji wengine wapya 5*, katika nafasi ya beki wa pembeni kulia/kushoto (1),  beki wa kati (1), kiungo wa kushambulia (1), na ushambuliaji (2).

Uongozi wa timu ya Ruvu Shooting Star,  katika kikao chake leo, August 5, 2020, umeridhia mapendekezo hayo ya benchi la ufundi, tayari umeanza utekelezaji.

Wachezaji walioachwa ni pamoja na *Zair Rajabu, Jamal Mnyate, Salum Makota, Edward Christopher na Adam Faraja*.

Masau Kuliga Bwire
Afisa Habari wa Ruvu Shooting Star.

SIMBA QUEENS 5-0 BAOBAB QUEENS, YAIVUA UBINGWA JKT QUEENS VIDEO: LIVE SAMATTA, MANARA NA ALIKIBA KUHUSU ISHU YA NIFUATE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply