Uncategorized

NAMUNGO WAMEDHAMIRIA KUSHUSHA MAJEMBE NANE YA KAZI, MMOJA KUTOKA YANGA

admin August 11, 2020 6:47 am

 


BAADA ya kuwa na uhakika wa kuwakilisha nchi kimataifa kwenye Kombe la Shirikisho, uongozi wa Namungo umesema kuwa utasajili wachezaji nane wa kazi.

Tayari Namungo imeshapata saini ya kiungo Fredy Tangalo aliyesaini kandarasi ya miaka miwili na inatajwa kuingia kwenye rada za kuwania saini ya nahodha msaidizi wa Yanga, Juma Abdul ambaye ni mchezaji huru baada ya mkataba wake wa kuitumikia Yanga kuisha.


Akizungumza na Championi Jumatatu, Mwenyekiti wa Namungo FC, Hassan Zidadu, alisema kuwa wameshaanza mchakato wa kusajili wachezaji wapya ili kukiongezea nguvu kikosi hicho.


“Tupo kwenye mpango wa kusajili wachezaji wapya na kila kitu kinaenda sawa kwa kuanza na kuwaongezea mkataba wale ambao muda wao umeisha pamoja na kuongeza wengine nane kwa mujibu wa ripoti ya Kocha Mkuu.


“Tutaiwakilisha nchi kimataifa, hivyo lazima usajili wetu uwe wa kimataifa zaidi ili tuweze kupeperusha Bendera ya Taifa, mashabiki wasihofie, tupo kamili,” alisema Zidadu.

NYOTA HUYU ALIYEKIPIGA ULAYA YUPO MBIONI KUTANGAZWA YANGA KUHUSU SAKATA LA BERNARD MORRISON, UJUMBE WA JEMBE HUU HAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply