Uncategorized

BEKI MPYA YANGA: NITAWASHANGAZA WENGI

admin August 12, 2020 6:47 am

 

BAKARI Mwamnyeto, beki mpya ndani ya kikosi cha Yanga, amesema kuwa atawashangaza wengi ndani ya kikosi hicho kwa kuwa wengi wanafikiri kwamba atashindwa kupata namba.

 

Mwamnyeto ni ingizo jipya ndani ya Yanga akisaini kandarasi ya miaka miwili kwa dau la milioni 220 ambapo inaelezwa kuwa milioni 70 aliziweka mfukoni mwake na milioni 150 zilikwenda Coastal Union.

 

Mwamnyeto alisema kuwa hana mashaka na suala la namba kwenye maisha mapya, anaamini uwezo wake na atawashangaza wengi.

 

β€œWengi wana mashaka nami ila tayari nimeshafungua ukurasa mwingine wa maisha, nitapambana kuwa bora na wengi hawataamini watakachokiona, nipo tayari kwa ushindani.

 

β€œNikiwa Coastal Union nimejifunza mengi pia nilicheza mechi nyingi ngumu na timu ilipata matokeo, hivyo hakuna haja ya kuwa na mashaka katika uwezo wangu,” alisema.

 

Kwa msimu wa 2019/20 Mwamnyeto alikuwa anawania tuzo mbili ambazo ni ile ya mchezaji bora na beki bora zote alikosa na kuibukia kwenye kikosi bora cha msimu wa 2019/20.

PIERRE ASAINI DILI LA MIAKA MITANO TOTTENHAM MTIBWA SUGAR YADAI KIBWANA ALIYESAJILIWA YANGA BADO NI MALI YAO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply