Uncategorized

AUBAMEYANG AKUBALI KUBAKI ARSENAL

admin August 18, 2020 6:47 am


NAHODHA wa Klabu ya Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang amekubali kusaini dili jipya la miaka mitatu ndani ya Klabu hiyo.

Nyota huyo alikuwa kwenye mpango wa kuondoka ndani ya kikosi hicho kilicho chini ya Kocha Mkuu, Mikel Arteta ila kwa sasa ameonyesha nia ya kubaki kuendelea kukitumikia kikosi hicho kwa ajili ya msimu wa 2020/21 na mshahara wake unatarajiwa kuwa pauni 250,000 kwa wiki.

Pia Arsenal inapiga hesabu za kupata saini ya beki wa Lille, Gabriel Maghalhaes ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho.

Arteta anahitaji kufanya mabadiliko makubwa ndani ya timu hiyo inayotumia Uwanja wa  Emirates ili kuwa na timu bora ndani ya Ligi Kuu England pamoja na michuano mingine. 

HIZI HAPA MECHI TANO ZA MWANZO ZA AZAM FC ALICHOFANYWA BEKI ALIYESAINI DILI JIPYA NA YANGA ACHA KABISA, MABOSI WAMPOTEZEA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply