Uncategorized

RASMI SASA, SENZO WA SIMBA NI MALI YA YANGA

admin August 20, 2020 10:47 am

 


UONGOZI wa Yanga, rasmi leo umemtambulisha Senzo Mbatha kuwa mfanyakazi wao ndani ya klabu hiyo akitokea Klabu ya Simba.


Senzo alijiuzulu nafasi yake ndani ya Simba hivi karibuni na kuzua mshtuko mkubwa kwa wanachama na viongozi wa klabu yake ya zamani kwa kuwa hawakujua anaweza kuibukia kwa watani zao wa jadi.


Akiwa ndani ya Simba, Senzo aliweza kuiongoza Simba kwa mafanikio makubwa na kusimamia usajili wa mchezaji wao nyota Luis Miqussone ambaye inaelezwa kuwa alikuwa kwenye hatua za mwisho kuibukia Yanga.

Sababu kubwa ya Senzo kusepa ndani ya Simba inaelezwa kuwa mkataba wake ulikwisha na mabosi wa Simba waligoma kumuongezea mkataba mwingine jambo lililomfanya bosi huyo abagwe manyanga kabla ya muda wake kuisha jumlajumla kwenye mkataba wake.


Leo, Agosti 20, Yanga wamemkaribisha kiongozi huyo Jangwani  rasmi ndani ya klabu hiyo ambayo kwa sasa inaboresha kikosi chake.

LUIS , KONDE BOY WA SIMBA KAENDA ZAKE KUOA SABABU YA TANZANIA PRISONS KUHAMISHIA MAKAZI YAO UWANJA WA NELSON MANDELA, RUKWA HII HAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply