Uncategorized

CHIRWA OBREY, SIMCHIMBA WAKIWASHA AZAM FESTIVAL

admin August 24, 2020 4:47 am

 



AZAM FC inayonolewa na Arstica Cioaba, jana Agosti 23 kwenye kilele cha Azam Festival iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Namungo FC kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Obrey Chirwa alianza kucheka na nyavu dakika ya 37 akimalizia pasi ya Nevere Tigere baada ya mabeki wa Namungo FC na kipa kujichanganya ndani ya 18 kiulaini akauzamisha mpira wavuni.

Steven Sey aliweka mzani sawa dakika 57 kwa kichwa matata akimalizaia pasi ya Edward Manyama.

Bao la ushindi lilipatikana dakika ya 66 kupitia kwa mshambuliaji wa Azam FC, Andrew Simchimba aliyekutana na mpira uliotemwa na kipa wa Namungo FC.


Tamasha hilo lilikuwa ni maalumu kwa ajili ya kutambulisha wachezaji wapya na wale waliokuwa ndani ya kikosi cha Azam FC kwa msimu wa 2019/20 ikiwa ni tayari kwa ajili ya Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza Septemba 6.

MO WA SIMBA AKUBALI USAJILI WA YANGA, MORRISON ATUMA UJUMBE, NDANI YA CHAMPIONI JUMATATU BAYERN MUNICH MABINGWA LIGI YA ULAYA, NEYMAR AMWAGA MACHOZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply