Uncategorized

KMC YACHWAPA MABAO 3-1 NA SIMBA

admin August 26, 2020 11:47 am

 


TIMU ya Simba leo Agosti 26 imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 mbele ya KMC kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Uhuru.


KMC ilianza kupachika bao la kwanza dakika ya pili kupitia kwa mshambuliaji wao mpya, Reliants Lusajo aliyekuwa akikipiga Namungo dakika ya pili.

Mabao ya Simba yalifungwa na kiungo Clatous Chama dakika ya 28 lile la pili lilipachikwa na Ibrahim Ajibu dakika ya 33 na msumari wa mwisho ulikomelewa na Mzamiru Yassin dakika ya 57.

Mchezo mwingine wa kirafiki ambao walicheza leo Simba ulikuwa ni dhidi ya Transti Camp ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 5-2.

Mechi zote zilichezwa Uwanja wa Uhuru ikiwa ni maandalizi kuelekea mchezo wa ngao ya jamii utakaochezwa Agosti 30 dhidi ya Namungo FC, Uwanja wa Sheikh Amri beid, Arusha ikiwa ni ufunguzi wa Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza Septemba 6.



SIMBA YAKUBALI MAJEMBE YA KAZI YA YANGA NAMUNGO FC WAJIPANGA KWA AJILI YA MECHI YA NGAO YA JAMII

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply