Uncategorized

MASHINE HII NYINGINE MPYA YA YANGA KUTUA LEO

admin August 26, 2020 8:47 am


 NYOTA mwingine wa Yanga ambaye yeye ni mshambuliaji anatarajiwa kutua leo Agosti 26 ili kujiunga na wachezaji wenzake ambao tayari wameshaanza mazoezi.

Nyota huyo raia wa Burkina Faso ni mshambuliaji anaitwa Yacouba Sogne na tayari alishamalizana na Yanga kwa kandarasi ya miaka miwili.

Wengine ambao ni washambuliaji waliomalizana na Yanga ni pamoja na Michael Sarpong raia wa Ghana na Wazir Junior yeye ni mzawa.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa nyota huyo alikuwa na udhuru kutokana na ‘lockdown’.

“Lockdown ambayo imesababishwa na janga la Virusi vya Corona ilikuwa inaendelea nchini kwao na ilifanya ashindwe kuja ila kwa sasa imeshaisha na tunatarajia anaweza kutua leo ili kuungana na wachezaji wenzake,” emesema.

REKODI ZA MESSI NA BARCELONA, KWA SASA HATAKI KABISHA KUBAKI HAPO AZAM FC: TUPO TAYARI KWA MSIMU MPYA WA 2020/21

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply