Uncategorized

MBWANA SAMATTA ACHEKELEA KUBAKI EPL

admin September 2, 2020 5:47 pm

 


NAHODHA wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta, ataendelea kukipiga katika Klabu ya Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu England.

 

Aston Villa imenusurika kushuka daraja msimu huu, baada ya kumaliza nafasi ya 17 katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 35. Timu hiyo ilifanikiwa kubaki baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na West Ham inayofundishwa na kocha David Moyes.

 

Samatta amesema:-. Napenda kumshukuru Mungu kwa kunipa nafasi nyingine tena, napenda kuwashukuru mashabiki waliokuwa nyuma yangu, kuiombea Villa kubaki msimu ujao, nawaomba waendelee kuomba ili na mimi niendelee kubaki hapa,” alisema Samatta.

 

Samatta alijiunga na Klabu ya Aston Villa akitokea Genk ya Ubelgiji kwa kitita cha pauni milioni 8.5 (zaidi ya sh bil. 25 za Tanzania).


Kwa sasa tayari Aston Villa imeanza maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu England inayotarajiwa kuanza Septemba 12.

SIMBA: KISINDA ATALETA UPINZANI NDANI YA LIGI KUU BARA BWALYA APEWA MCHONGO SIMBA, YANGA WAMEANZA, KESHO NDANI YA SPOTI XTRA ALHAMISI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply