Uncategorized

RUVU SHOOTING YATUMA UJUMBE HUU KWA IHEFU FC

admin September 10, 2020 12:47 pm


 UONGOZI wa Ruvu Shooting umesema kuwa umejipanga kuvunja rekodi waliyoweka msimu uliopita kwa kumaliza ligi wakiwa nafasi ya 12 na pointi zao 47 baada ya kucheza mechi 38 za ligi.

Mchezo wa kwanza Ruvu Shooting inayonolewa na Kocha Mkuu, Charles Mkwasa iligawana pointi moja na Mtibwa Sugar, Septemba 6, Uwanja wa Gairo kwa sare ya bila kufungana.

 Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa kuanza kwa sare kumewapa nguvu ya kujipanga na kuyafanyia kazi makosa yao.

“ Tulitawala mchezo dhidi ya Mtibwa ila tulishindwa kutumia nafasi ambazo tulizipata, tunakwenda kupambana na Ihefu,hilo tunalitambua  tupo vizuri na tunahitaji ushindi hakuna jambo jingine.

“Mchzo wetu utakuwa na ushindani hilo lipo wazi ila tumejipanga. Leo timu itaanza safari kuelekea Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya timu kushuka uwanjani,” amesema Bwire.

Ihefu ambayo imepanda Ligi Kuu Bara msimu huu itakutana na Ruvu Shooting, Uwanja wa Sokoine ikiwa na kumbukumbu ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 mbele ya Simba, Septemba 6.

MUONEKANO wa ukurasa wa mbele wa Gazeti la SPOTI XTRA Alhamisi, lipo mtaani, jipatie nakala yako kwa Tsh 500 tu. KAGERE AMESHINDIKANA BONGO,CHIRWA, SARPONG WAKWAMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply