Uncategorized

SIMBA YAZITAKA POINTI TATU ZA MTIBWA SUGAR

admin September 11, 2020 5:47 am

 

UONGOZI wa Simba umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa Septemba 12, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. 

Tayari kikosi cha Simba kimeshatia timu ndani ya Moro na jana Septemba 10 walianza mazoezi kwa ajili ya kujiweka fiti kumenyana na wapinzani wao.

Ofisa Habari wa Simba,  Haji Manara amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya ushindani na wanahitaji pointi tatu muhimu.

Simba inakutana na Mtibwa Sugar iliyotoka kulazimisha sare ya bila kufungana na Ruvu Shooting mchezo wa kwanza Uwanja wa Gairo Moro, huku wao wakishinda kwa mabao 2-1 mbele ya Ihefu,Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Msimu uliopita walipokutana Uwanja wa Jamhuri,  Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 na ule wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru Simba ilishinda mabao 2-1.

YANGA YAIPIGIA HESABU MBEYA CITY CHELSEA WAIPOTEZA INTER MILAN KWA KANTE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply