Uncategorized

AZAM FC WAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA MBEYA CITY

admin September 16, 2020 10:47 am

 


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Septemba 20, Uwanja wa Sokoine Mbeya dhidi ya Mbeya City. 


Mchezo huo utakuwa ni wa kwanza kwa Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Aristica Cioaba kucheza nje ya Dar kwa kuwa mechi zote mbili ilicheza pale Uwanja wa Azam Complex. 


Imecheza mechi mbili na kushinda zote ilianza mbele ya Polisi Tanzania,  Septemba 7 kwa ushindi wa bao 1-0 kisha ilishinda mabao 2-0 mbele ya Coastal Union.


Ofisa Habari wa Azam FC,  Zakaria Thabit amesema kuwa kwa sasa wachezaji wote wapo tayari kwa ushindani na lengo ni kufikia malengo ambayo wamejiwekea.


“Tunaamini kwamba kuanza kwa ushindi kwenye mechi zetu za awali ni mwanzo mzuri, tunatambua kwamba kuna mechi nyingine ngumu ila tutapambana kupata matokeo chanya,” amesema. 


Mbeya City itakuwa nyumbani ila kwa mara ya kwanza baada ya kuyeyusha pointi sita ugenini ilianza kupokea kichapo cha mabao 4-0 mbele ya KMC kisha ikapoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Yanga.

BERNARD MORRISON KUKUTANA NA BALAA LA SARPONG KCB YASAINI MKATABA WA MWAKA MMOJA KUDHAMINI LIGI KUU TANZANIA BARA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply